MADAKTARI BINGWA KUWEKA KAMBI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA

Posted on: April 23rd, 2024

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea, Dkt Magafu Majura amesema kuwa wanatarajia kupokea jopo la madaktari bingwa kutoka Hospitali za Rufaa za mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo Ruvuma, Njombe, Mbeya na Songwe.

Akizungumza mapema hii leo 23/04/2024 ofisini kwake amesema kuwa wanatarajia kupokea madaktari bingwa ambao watatoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO).

Dkt Majura amesema katika kambi hiyo kutatolewa huduma mbalimbali za kibingwa za akina mama na uzazi, huduma za magonjwa ya watoto, hudumaza kibingwa za magonjwa ya ndani kama vile kisukari, shinikizo la damu, figo na moyo, huduma za upasuaji na mifupa, huduma za macho, huduma za Afya ya akili, huduma za kinywa na meno, huduma za masikio, pua na koo, huduma za ngozi, huduma za mfumo wa chakula, huduma za moyo kwa watoto, huduma za saratani.

“Kutotana na uhaba wa huduma hizo Wananchi wamekuwa wakihangaika kufuata matibabu ya kibingwa mbali hivyo Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassani kupitia wizara ya Afya kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Ruvuam imesogeza huduma karibu  ili kuondoa usumbufu kwa Wananchi” amesema Dkt Majura

Pia amesma ujio wa madaktari hao utakuwa ni fursa kwa wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO) kwakuwa watawajengea uwezo wataalamu waliopo.

Dkt majura amewahimiza wananchi kufika na kupata huduma ambazo  zimeongezewa nguvu Pia amesema kutakuwepo na wataalamu wa huduma za mionzi za damu za usingizi na ganzi.

Bahati Omary mkazi wa Songea mjini amesema kuwa ujio wa madaktari hao utasaidia watu wenye magonjwa mbalimbali ambao wanahitaji huduma za kibingwa

“Binafsi nimesikia tangazo la ujio wa madaktari hao kwangu ni fursa kubwa nawahimiza na wengine waione fursa hii muhimu ambayo inaenda kutuokoa na kutupa nafasi ya kuwa wenye Afya nyema” amesma Omary