RAS RUVUMA AIPONGEZA HOSPITALI YA RUFAA SONGEA KWA UTOAJI HUDUMA BORA KWA WANANCHI
Posted on: September 3rd, 2024Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bi Mary Makondo ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea kwa kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na maeneo ya jirani
Pongezi hizo amezitoa alipokuwa akizungumza kwenye kikao kazi na Watumishi wote wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea, kilichofanyika leo tahere 3/09/2024 katika ukumbi wa Hospitali.
“Natambua na nina wapongeza sana kwa majukumu makubwa ya kipekee mnayo yafanya kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na watanzania wote kwani jukumu mlilopewa ni kuweza kuhudumia wananchi katika kuimarisha afya zao ”
Amesema Serikali imeendelea kutoa fedha kwa lengo la kuboresha sekta ya afya kwa kuwezesha upatikanaji wa Huduma bora za matibabu, miundo mbinu na vifaa tiba vya kisasa hizo zote ni juhudi za serekali ili wananchi waweze kutekeleza majukumu yao ya kiuchumi na kijamii katika ujenzi wa taifa.