Afya Ya Jamii
Posted on: October 25th, 2019Afya Ya Jamii
Jifunze njia za kujikinga na maambukizi ya Ebola.
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola :
Epuka kusalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana
Epuka kugusa damu, matapishi, mkojo, kinyesi, kamasi, mate, machozi na maji maji mengine yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za ugonjwa huu
Epuka kugusa au kuosha maiti ya mtu aliyekufaakiwa na dalili za ebola badala yake toa taarifa kwa uongozi wa serikali ili wasimamie taatibu za mazishi
Epuka kutumia nguo, shuka, blanketi, kitanda nagodoro za mtu aliyeambukizwa ugonjwa, toa taarifa kwenye ofisi za serikali ya eneo husika
Kwa kuwa ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja
Nawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni mara unapomtembelea mgonjwa hospitalini au kumhudumia nyumbani
Epuka kugusa wanyama kama vile Popo, Nyani, Sokwe, Tumbili na Swala au mizoga ya Wanyama
Zingatia ushauri na maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na viongozi wa serikali.
Wahi kituo cha kutolea huduma za afya uonapo dalili za ugonjwa wa Ebola
Toa taaifa mapema kwa watoa huduma za afya uonapo mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola au kifo
Zingatia usafi binafsi pamoja na usafi wa mazingira yako.