MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI AONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA JENISTA MHAGAMA

Posted on: December 14th, 2025


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameongoza waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, leo Desemba 16, 2025 yaliyofanyika Kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Akizungumza baada ya mazishi, Dkt. Nchimbi amesema Taifa limepoteza kiongozi wa mfano aliyewatumikia wananchi kwa dhati, unyenyekevu na kujitoa bila kuchoka.