NAIBU WAZIRI WA AFYA ASHIRIKI MAZISHI YA JENISTA MHAGAMA

Posted on: December 16th, 2025


Pichani wanne kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Florence Samizi kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ameshiriki mazishi ya Marehemu Jenista Mhagama aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho.

Mazishi hayo yameongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo desemba 16, 2025 katika Kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma.