RC RUVUMA AWASISITIZA WAHUDUMU WA AFYA KUFANYA KAZI KWA WELEDI.
Posted on: November 15th, 2025Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, ametoa wito wa wataalamu wa Afya kutoa huduma kwa waledi, upendo, kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za nchi na miiko ya kazi zao.
Ametoa wito huo wakati akifingua kambi ya madaktari Bingwa na Bozezi wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto na watu wazima na Madaktari bingwa wa upasuaji wa Fistula katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO).
Ametoa wito kwa wananchi kuzingatia maelekezo ya wataalamu juu ya kujikinga na Magonjwa ya Moyo ambayo yanazuilika kwa kubadilisha tabia za ulaji wa Vyakula bora na kufanya mazoezi.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea, Dkt. Magafu Majura ametoa shukurani kwa taasisi ya hospitali ya Benjamin Mkapa na chama cha madaktari bingwa wa upasuaji wa fistula Tanzania kwa kuleta kwa kusogeza karibu huduma za kibingwa Kwa wananchi.
Ameeleza kuwa ujio wa madaktari hao utawanufaisha wataalam wa mkoa wa Ruvuma na kuwajengea uwezo ambao utawawezesha kutoa huduma stahiki na kwa wakati.



