SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA JENISTA MHAGAMA RUVUMA

Posted on: December 14th, 2025


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ameongoza viongozi na maelfu ya waombolezaji kupokea mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama, ulipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea, mkoani Ruvuma.

Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komred Oddo Mwisho.
Mapokezi hayo yamegusa hisia za wengi, yakionesha heshima ya kitaifa kwa kiongozi aliyekuwa na mchango mkubwa katika uongozi na utumishi wa Umma.