WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA IBADA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU JENISTA MHAGAMA

Posted on: December 15th, 2025


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Mhe. Jenista Mhagama alikuwa kiungo kati ya kanisa na Serikali amefanya kazi hiyo ya mahusiano, Serikali itaendelea kuenzi na kushirikiana na taasisi za dini ili kuweza kuhakikisha kwamba heshima kubwa ambayo Tanzania imekuwa nayo kuhusu umoja wa kitaifa uhuru wa kuabudu, amani na usalama wa nchi yetu unaendelezwa.

Ameyasema hayo, wakati akitoa salamu za pole baada ya ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jenista Mhagama ambayo imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Benedict, Abasia ya Peramiho, katika Jimbo kuu la Songea, Desemba 15, 2025.

Waziri Mkuu ameendelea kuelezea mema ya Marehem Jenista Mhagama aliyoyafanya kipindi cha uhai wake, alikuwa ni mpatanishi katika Nyanja mbalimbali akiwa Waziri wa Nchi amefanya kazi kubwa pale ambapo palionekana na dosali kati ya wafanyakazi na Serikali alirekebisha hadi leo watumishi wa umma na Serikali wanaushirikiano mkubwa.

“Mhe. Jenista Mhagama alifanya kazi ya kuweka ushirikiano na umoja kati ya Sekta binafisi na Serikali na jambo hiyo alilifanya kwa uadilifu na kwa jitihada kubwa” Amesema Mhe. Dkt. Nchemba.

Mhe. Dkt. Nchemba amemalizia kwa kusema Marehem Jenista Mhagama ni mtu aliyeamini kwamba ukimtanguliza Mungu na ukafanya bidii inawezekana.