CHAMA CHA MZIKI WA ASILI NA UMOJA WA WASANII SONGEA WAFANYA USAFI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA
Posted on: November 14th, 2025
Katibu Mkuu wa Chama cha Mziki wa Asili Tanzania, Mwl. Alexander Ngonyani amesema wameshirikiana kati ya Chama cha mziki wa asili Tanzani tawi la Songe pamoja na umoja wa wasanii Songea (UWASO) kwa ajili ya kutoa elimu na hamasa kuhusu usafi na utunzaji wa mazingira.
Ameyasame hayo baada ya shughuli ya kufanya usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea.
“Wasanii huwa tunatoa elimu na hamasa kupitia shughuli za sanaa mziki, nyimbo, maigizo na ngoma za asili, leo tumeamua kuja hapa Hopitali ya Rufaa ya Mkoa Songea kufanya usafi kwa vitendo" amesema Mwl. Ngonyani.
Mwl. Ngonyani ameyataja malengo yao makubwa ni kutoa elimu na hamasa kwa vitendo badala ya wao kama wasanii kuimba na kuigiza tu kutoa elimu kwa njia ya nadhalia.
Kwa upande wake Mhasibu wa Umoja wa Wasanii Manispa ya Songea (UWASO), Aviter Chiwango amesema lengo ni kuweka mazingira katika hali ya usafi na kuangalia ulinzi salama kwenye usafi kuhamasisha watu wasitupe taka ovyo vile vile kutotililisha maji ovyo ili kulinda Afya zeo.



