MATIBABU YA FISTULA NA MSAMBA YATATOLEWA BURE HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA (HOMSO) KUANZIA TAREHE 13/11/2025 HADI 21/11/2025

Posted on: October 21st, 2025



Chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Fistula Tanzania ( AOFST) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya. Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea na shirika la Fistula Foundation, wanatarajia kutoa matibabu ya Fistula na kuchanika msamba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea kuanzia tarehe 13/11/2025 hadi 21/11/2025.




Matibabu haya ni Bure nauli na chakula vitatolewa kwa wagonjwa wote. Wakina mama wote wanaosumbuliwa na Fistula ama waliochanika msamba wakati wa kujifungua kutoka katika Mkoa wa Ruvuma na mikoa ya jirani mnakaribishwa kupata matibabu haya.