TAKUKURU YAKABIDHI MASHINE ZA WATOTO WACHANGA HOMSO

Posted on: October 11th, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Ruswa (TAKUKURU) Crispin Chalamila amekabidhi mashine mbili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea kwa ajili ya kutengeneza joto kwa watoto wachanga hasa watoto njiti na matibabu ya ugonjwa wa manjano kwa watoto.

Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea leo tarehe 12/10/2025.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Crispin Chalamila, amesema vifaa wavyokuja navyo ni kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suruhu Hassani katika kuimalisha na kuboresha huduma za Afya kwa watanzania wote.

“ Tumechagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea kwa sababu tunaamini wagonjwa wakishindikana Wilayani wataletwa hapa Rufaa kwa zawadi hii wataweza kunufaika wakazi wote wa Mkoa wa Ruvuma”, amesema Chalamila.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto HOMSO, Dkt. Regina Hyera amesema vifaa hivi vitawasaidia kutatua changamoto kubwa wakitazama watoto wanaolazwa mle asilimia 43 ya watoto ni njiti chini ya kg mbili na nusu ndio wanaohitaji joto na katika vifaa walivyowaletea kuna kifaa maalumu ambacho ni Infant Radiant Warmer kitakacho msaidia mtoto kutunza joto lake la mwili.

Dkt. Hyera amewashukuru TAKUKURU kwa vifaa tiba walivyowaletea kwani vimelenga huduma muhimu za watoto wachanga hivyo wameunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza vifo vya watoto wachanga ambao ndio taifa la kesho.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Louis Chomboko ametoa shukrani kwa TAKUKURU msaada waliotoa ni wathamani kubwa TAKUKURU kushirikiana na Serikali katika kuimarisha ustawi wa wananchi na kutoa mchango Chanya katika Sekta ya Afya vifaa hivi vitaboresha huduma za Afya kwa Watoto wachanga, kupunguza vifo vya Watoto wachanga na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea.

Kwa upande wake Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda amesema eneo lenye ushirikiano kati ya TAKUKURU na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea kwenye ukaguzi wa Miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Sekta ya Afya HOMSO wamekuwa wakiwapatia ushirikiano wa hali ya juu.