TRA MKOA WA RUVUMA WATOA SHUKRANI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA
Posted on: August 13th, 2025
Meneja msaidizi wa ukaguzi Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Ruvuma Mabula Mayiku ametoa shukrani ya mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea, ikiwa ni sehemu ya Faraja kwa wagonjwa.
Shukrani hiyo ameitoa wakati akiendelea na zoezi la kukabidhi mahitaji ya shukrani ambayo yametolewa katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea.
Mayiku amesema wanautamaduni kila mwisho wa mwaka wa fedha huwa wanarudisha shukrani kwa wananchi wenye uhitaji mwaka huu wameona vyema kuja kutembelea wahitaji ambao ni wagonjwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea,
“ Tumekuja na vitu mbalimbali kwa ajili ya kutoa shukrani zetu tuna mashuka, Sukari, Unga, Mafuta, vifaa vya usafi (pipa la taka, mifagio), mchele vitu vyote vina thamani ya shilingi milioni tatu”, amesema Manyiku.
Lengo ni kutoa shukrani kwa wateja wao ambao ni walipa kodi wanaowawezesha wao kufanya kazi zao kwa wepesi zaidi.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea Dkt. Magafu Majura, ametoa shukrani kwa uongozi na watumishi wote wa TRA Mkoa wa Ruvuma kwa shukrani zao ambazo wamezikabidhi kwao kwa ajili ya wagonjwa na kwa ajili ya shuguli ya usafi ndani ya Hospitali.
Vile vile Dkt Majura amesema kunawagonjwa ambao ni walipa kodi kwahiyo watakapokuwa wanahudumiwa chakula hiki ambacho kimetolewa wataweza kupona kwa haraka na kurudi katika majukumu yao ya kawaida ya kujizarishia mali ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye ulipaji wa kodi pia na watumishi wa Hospitali ni walipa kodi kwa njia mbalimbali wanashukuru sana kunufaika na shukrani hii ambayo TRA wameirudisha kwa wananchi.