WATUMISHI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA WASISITIZWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI KAZINI

Posted on: April 17th, 2024

Watumishi wa Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO) wasisitizwa kujenga mahusiano mazuri baina yao na wagonjwa  wakati wote wanapotoa huduma ya matibabu.

Wito huo umetolewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea Dkt Magafu Majura leo Aprili 16, 2024 katika kikao cha robo ya pili kilichowakutanisha watumishi wote kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya uboreshaji huduma kwa wateja.

Dkt Majura Amesema kufanya kazi kwa weledi pamoja na kusimamia taratibu na sheria katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa itasaidia kutekeleza vyema majukumu yao

Amesema kujenga mahusiano mazuri kazini  itasababisha kuiletea sifa nzuri taasisi hivyo amesisitiza matumizi bora ya lugha wakati wa kuhudumia wagonjwa kwani itaongeza mapato

“Lazima mzingatie matumizi ya lugha ya staha kwa  wagonjwa ili kuendeleza mahusiano baina yetu na wao pia tuwaone kama ndugu zetu tuliowaacha nyumbani kwani itasaidia sana katika ufanyaji kazi wetu”