WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SONGEA WAKUMBUSHWA KUTOA HUDUMA BORA

Posted on: June 9th, 2024

Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Hilda Ndambalilo amewataka na kuwahimiza Wauguzi wote mkoani Ruvuma kuzingatia Kanuni na maadili ya kazi ili kulinda taaluma zao na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa jamii.

Hayo ameyazungumza kwenye kikao na Wauuguzi wote wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea (HOMSO) kilichofanyika katika ukumbi wa HOMSO.

Ndambalilo amesema lengo la kikao hicho ni kukumbushana kuhusu maadili ya kazi kwa mtoa huduma za afya ambayo yatamuongoza kutunza staha, utu na heshima ya mgonjwa.

“Mambo makubwa ambayo tumeelekezana kupitia kikao hiki ni kufanya kazi kwa kufuata miongozo na kanuni za kazi ambazo niwajibu wa kila mtoa huduma wa afya ili mwisho wa siku tuboreshe huduma zetu ”amesema Ndambalilo